More quotes by Enock Maregesi

"Imani ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana na hupeleka watu kwenye ukweli. Kuamini hupotosha, na ni nia ya kudharau kinachoweza kujulikana."
"Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote; au 'pushing the envelope' kwa lugha ya kigeni."
"Yusufu alikuwa hohehahe kabla na baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa, hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo utakaotutafuta sisi."
"Kuikaribisha amani ya Mungu katika maisha yangu kumenisaidia. Naishi mbinguni duniani."
"Wasifu wa viongozi wa Kolonia Santita ni siri kwa sababu siri ni siri ya mafanikio."